Habari ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) – ABNA: Katika ulimwengu wa imani na hadithi, daima kumekuwa na simulizi kuhusu nguvu za giza na wafuasi wa shetani; viumbe vinavyojificha katika kivuli na kutekeleza misheni maalum ya kuanzisha ushawishi na upotovu. Lakini hawa wafuasi ni nani na ni nafasi gani wanayoikalia katika dunia yetu? Ikiwa una hamu ya kufichua siri za nguvu hizi zisizojulikana, jiunge nasi.
-
Walahan
Anamshawishi mwanadamu katika usafi na sala, na kumfanya aamini kuwa sala hiyo haiko sahihi. -
Hafaf
Analenga kuogopesha mwanadamu jangwani na jangwani kumnyanyasa kwa hofu au kuonekana kwa mwanadamu kama wanyama wa aina mbalimbali. -
Zalambur
Anasimamia wafanyabiashara. Anapamba maneno ya uongo na uwongo mbele ya mwanadamu. -
Thabr
Wakati maafa yanapomkuta mwanadamu, anafanya kuwa kuvunjika kwa uso, kujipiga, kuchoma shingo na mavazi kunakubalika. -
Abyad
Anahusika kumkasirisha mwanadamu na kufanya hasira ionekane halali, na kwa njia hiyo damu inamwagika. -
A’war
Ni shetani aliye kushawishi mpendwa wa ibada kufanya zina na binti fulani. -
Dasim
Daima anasimamia nyumba. Wakati mwanadamu anaingia ndani ya nyumba bila kusema salaam au kutamka jina la Mungu, anakuwa pamoja naye ndani ya nyumba na kumshawishi hadi kuleta shari na fitina. -
Mutrash
Kazi yake ni kueneza habari za uongo na uzushi. -
Qandhir
Anasimamia maisha ya watu. Hivyo mwanadamu anakuwa mpweke na hafahamu haki za familia yake. -
Dahhar
Misheni yake ni kumuumiza Muumini wakati wa usingizi. -
Qabdhi
Kazi yake ni kuweka mayai. Kila siku anaweka mayai 30: 10 mashariki, 10 magharibi, na 10 ardhini; kutoka kila yai hutoka wafuasi wa shetani, majini na majitu ambao wote ni maadui wa mwanadamu. -
Tamrih
Imam Sadiq (a.s) alisema: Kwa Iblis, msaidizi wake katika kupotosha watu aliyeitwa (Tamrih) anafanya kazi kati ya magharibi na mashariki mwanzoni mwa usiku, kwa kuwatia watu wasi wasi na kuujaza wakati wao (kwa kuwashughulisha na mambo yasiyokuwa na faida). -
Qaz'h
Ibn Kawa aliuliza Amirul Mu’mineen (a.s) kuhusu Qaws na Qazah; Bwana alisema: “Usiuse Qaws Qazah, kwa sababu ni jina la shetani (Qazah), badala yake useme Qaws Allah na Qaws Ar-Rahman.” -
Zawal
Kwa wanaume walio na ugonjwa unaojulikana katika maandiko kama (ugonjwa wa ibnah - au ugonjwa wa mtoto wake, kwa maana ugonjwa huu ni ugonjwa wa kimagical au wa roho unaoshirikishwa au kuhusishwa na mtoto wa shetani, na siyo ugonjwa wa kawaida wa kimatibabu. Kwa ibara nyingine: Ugonjwa unaojulikana kwa istilahi ya Ugonjwa wa Mwanawe (مرض ابنه) ni ugonjwa maalumu unaohusiana na mwana wa Iblis aliyeitwa Zawal, ambao mara nyingi huathiri wanaume fulani), Zawal mwana wa Iblis hushirikiana nao wanaume hao, na waliokumbwa huwa wanaathirika na ugonjwa huo. -
Laqis
Huyu ni mmoja wa mabinti wa shetani, kazi yake ni kuwasukuma wanawake kufanya mapenzi ya jinsia moja. -
Mutakawwin
Anabadilisha sura yake na kudanganya watu. -
Madhhab
Anajionyesha (anajidhihirisha) kwa sura mbalimbali isipokuwa Sura ya Mtume au Khalifa wake; na anafanya kazi ya kuwapotosha watu kwa kila njia anayoweza. -
Khanzab - (خنزب)
Anavuruga sala ya mwenye kusali; yaani, anavuruga umakini wa moyo wake na kujaribu kumtoa katika sala yake. -
Muqlas
Anasimamia kamari. Wachezaji wote kamali wanatimiza amri zake. Ukiona mtu anahangaika na kamali ujue ni mtumishi huyo wa shetani ndio anamuelekeza na yeye anatii amri zake. -
Tartabah (طرطبة)
Ni moja ya binti wa laana. Kazi yake ni kuwasukuma wanawake kufanya zinaa na pia kuwaleta katika mapenzi ya jinsia moja.
Tamko la Majina hayo kwa Kiarabu:
1- ولهان (Walahan)
2- هفاف (Hafaf)
3- زلنبور (Zalambur)
4- ثبر (Thabr)
5- ابيض (Abyad)
6- اعور (A’war)
7- داسم (Dasim)
8- مطروش (Mutrash)
9- قنذر (Qanadhir)
10- دهار (Dahhar)
11- قبض (Qabd)
12- تمریح (Tamrih)
13- قزح (Qazah)
14- زوال (Zawal)
15- لاقيس (Laqis)
16- متکون (Mutakawwin)
17- مذهب (Madhhab)
18- خنزب (Khanazb)
19- مقلاص (Muqlas)
20- طرطبه (Tartabah).
Chanzo: Safinat al-Bihar, Juz’i la Kwanza, uk. 99-100
Your Comment